Baki na pesa yako tiketi zimeisha

DAR ES SALAAM :Klabu ya Simba imemaliza uuzaji wa tiketi zote kwa siku tatu kuelekea siku kilelele cha tamasha lijulikanalo kama “Simba Day” litakalofanyika siku ya tarehe 3 Agosti 2024.
Taarifa hizo zimenukuliwa kwenye Mtandao wa kijamii wa Klabu hiyo zikisema kuwa Afisa Mkuu,Imani Kajula amesema
“Hongereni sana mashabiki wetu na tukutane uwanja wa mkapa kwenye Simba Day ya Ubaya Ubwela. Timu yeyote kubwa inapimwa na ukubwa wa sapoti ya mashabiki wake, na hii inadhihirisha kwanini mashabiki wa Simba mlichaguliwa kuwa mashabiki bora barani Afrika.”Amesema Kajula
Kauli mbiu ya Klabu hiyo ni ” UBAYA UBWELA”



