Balozi Dk Suleiman akutana na watanzania UN New York

KAIMU Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Dk Suleiman Haji Suleiman amekutana na kufanya mazungumzo pamoja na tafrija ndogo na Watanzania wanaofanya kazi katika Umoja wa Mataifa jijini New York nchini Marekani.
Mazungumzo hayo yamefanyikakatika Ofisi za Uwakilishi New York.
Aidha, Balozi Dk Suleiman amewashukuru akuwapongeza Watanzania hao kwa kuwa mabalozi wazuri wanaoiwakilisha Tanzania ndani ya Umoja wa Mataifa.

Wafanyakazi hao wameushukuru uwakilishi kwa kuwaalika na kutenga muda wa kuwasikiliza na kuweza kusalimiana.
Vile vile mkutano ulizungumzia fursa za ajira, mafunzo na uwekezaji zilizoko ndani ya UN na kukubaliana kusaidia kuwasaidia Watanzania wengi zaidi kujua fursa hizo wenye nia ya kufanya kazi katika Umoja wa Mataifa Marekani.
Ghafla hiyo ilihudhuriwa na maofisa mbalimbali na ubalozini hapo



