Balozi Mahmoud aapishwa ubunge

DAR ES SALAAM: SPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson amemtaka Mbunge Balozi Mahmoud Thabit Kombo kumbeba Rais Samia Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza ipasavyo majukumu aliyopewa kwakuwa ni wachache walioaminiwa ili kubeba maono ya Mkuu huyo wa Nchi.

Dk. Tulia ameyasema hayo leo katika Ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam katika hafla fupi ya kiapo cha uaminifu kumuapisha Balozi Kombo aliyeteuliwa na Rais Samia kuwa Mbunge na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki mnamo Julai 21, 2024.

“Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linakutakia heri katika majukumu yako mapya utakayoanza kuyatumikia baada ya kuapishwa na Mheshimiwa Rais hapo kesho pia tunamtakia heri Rais katika shughuli zake za kulitumikia taifa ,” amesema Dk. Tulia.

Advertisement

Rais huyo wa Umoja wa Mabunge ametoa ufafanuzi wa kiapo hicho kwa kusema ni kwa mujibu wa Matakwa ya Ibara ya 68 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema Dk. Tulia.

“Fasili ndogo ya pili ya kanuni za Bunge zinampa nafasi Spika kuamua mahali popote pakuapisha,” amesema.

Viongozi kadhaa wamehudhuria hafla hiyo akiwemo, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Stergomena Lawrence Tax, Mbunge wa Jimbo la Mikumi, Dennis Londo aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki.

SOMA: Mahmoud Thabit Kombo: Safari ya Maisha na Kazi

Kabla ya uteuzi na uapisho huo, Balozi Kombo alikuwa ni Balozi wa Tanzania nchini Italia. Balozi Kombo anachukua nafasi ya Mbunge wa Jimbo la Bumbuli, January Makamba ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

/* */