BARAZA la Wafanyakazi la Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) limekutana leo kutathmini huduma zimazotolewa na hospitali hiyo ya rufaa ya kanda iliyopo jijini Dodoma.
Baraza ambalo limeketi chini ya uenyekiti wa Mkurugenzi Mtendaji wa BMH, Dk. Alphonce Chandika, limefanya tathimini ya huduma ili kuongeza ufanisi.
Baraza limeketi kwa mujibu wa Sheria za Utumishi wa Umma, ambayo inataka kila taasisi ya Umma ya kuwa na Baraza la Wafanyakazi. Baraza la Wafanyakazi ndiyo chombo cha juu sana katika ushirikishwaji wa wafanyakazi mahali pa kazi.