Barcelona yafuatilia “hali ngumu” ya Rafael Leao

Winga wa kushoto wa AC Milan, Rafael Leao.

KWA mujibu wa tetesi za usajili klabu ya Barcelona imeripotiwa kufuatilia “hali ngumu” ya mlengwa wake wa muda mrefu wa uhamisho Rafael Leao inayomkabili msimu huu katika timu ya AC Milan.

Leao amekuwa muhimu katika klabu ya Milan tangu alipojiunga mwaka 2019 lakini ghafla amejikuta si muhimu katika wiki za hivi karibuni kufuatia uvumi wa kutokuwa na maelewano mazuri na kocha Paulo Fonseca.

SOMA: Tetesi za usajili Ulaya

Advertisement

Mtandao wa michezo, SPORT umesema awali Barcelona ilianzisha ni kwa Leao kumsajili wakati wa dirisha la uhamisho majira ya kiangazi yaliyopita wakati uhamisho wa mlengwa mkuu wa usajili Nico Williams alipokwama.

Milan haikuwa tayari kumuuza Leao huku Barca ikijaribu kumsajili kupitia kwa wakala Jorge Mendes.

Sasa inasemekana kwamba Leao anachoka na hali yake, huku Barcelona ikitumaini kuwa itamchochea kuingia sokoni kwa bei inayofaa zaidi.

Imetafsiriwa kutoka 90min