Basata yatoa wito wasanii kuchangia waathirika Hanang

BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limetoa wito kwa wasanii kuungana kuchangia familia zilizoathirika na mafuriko na maporomo ya tope katika mji wa Katesh wilayani Hanang mkoani Manyara.

Katika maporomoko hayo yaliyotokea mwanzoni mwa wiki hii, kuna watu waliopoteza maisha, wengine wamejeruhiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Katibu Mtendaji wa Basata Dk Kedmon Mapana alisema wako tayari kuwasindikiza wasanii wanaotaka kutoa mchango wao kwa waathirika.

Advertisement

“Kama Basata tunatoa pole kwa wananchi wa Hanang kwa ujumla, lakini tunaamini kuwa kule kulikuwa na wasanii na wapo walioathirika kwa namna moja au nyingine,”

“Niwaombe wasanii wote nchini tuungane kwa pamoja tuweze kutoa michango kusaidia familia zilizoathirika, ni wakati wa kuwakimbilia wenzetu. Tuko tayari kuwasindikiza kule Hanang kutoa msaada, kwa hiyo tujitojeze kwenye shida na raha,”alisema.

Dk Mapana alisema Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza nguvu zote kwa sasa zielekezwa kule ili wananchi wa kule wajue kuna wenzao wenye uwezo wa kuwakimbilia.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *