‘Beetroot’ sasa kutengenezwa mvinyo

DAR ES SALAAM;  Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), imeliongezea thamani tunda la beetroot, ambapo sasa linatengenezwa mvinyo.

Mratibu wa Utafiti Kitaifa wa Mazao ya Mbogamboga, kutoka Kituo cha Tengeru Arusha, Emmanuel Laswai amesema kinywaji hicho kilichotengenezwa kina mchanganyiko pia wa mdalasini na tangawizi.

Soma: Vinywaji, Urembo kuchangia Bima ya afya kwa wote

Amesema tunda hilo lina kiasi kikubwa cha virutubisho, ambapo mtumiaji anapata kiwango kikubwa cha madini ya chuma.

” Kwa kutumia kinywaji hiki kinaburudisha, pia kinawezesha mwili kupambana na magonjwa,” amesema.

 

Habari Zifananazo

Back to top button