Chakula cha ziada chafikia tani milioni 5

TANGA: Kutokana na uboreshwaji wa mifumo ya uzalishaji wa chakula ikiwemo utafiti, imewezesha nchi kuwa na ziada ya chakula zaidi ya tani milioni 5 katika kipindi cha msimu wa 2024/25

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Dk Stephen Nindi alipozungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Tanga.

Amesema kuwa mafanikio hayo yametoka na ongezeko la bajeti ya wizara hiyo ambayo imewezesha kuboresha mifumo ya uwagiliaji,ruzuku za pembejeo kwa wakulima sambamba na utoaji wa chanjo ya mifugo.

“Utoaji wa ruzuku hizo umesaidia ongezeko la uzalishaji wa mazao kutoka tani milioni 18.9 mwaka 2021 hadi kufikia tani milioni 22 mwaka huu,”amesema Naibu Katibu Mkuu huyo.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk Batlida Burian amesema kuwa mkoa unaendelea kusimamia kwa ukamilifu mpango wa serikali wa uzalishaji wenye tija.

“Katika msimu wa kilimo wa mwaka 2024/25 takribani tani milioni 2 za mazao ziliweza kuzalishwa huku mahitaji halisi ya mkoa yakiwa ni tani 621,025

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button