Beijing Washington tafuteni njia ya maelewano

CHINA : RAIS wa China Xi Jinping amesema Beijing na Washington ni sharti zitafute njia ya maelewano ili kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizi mbili.

Kwa mujibu wa taarifa  iliyotolewa na shirika la utangazaji la China, CCTV. XI Jinping amesema China na Marekani hunufaika kutokana na ushirikiano mzuri baina ya nchi hizi mbili lakini endapo wanapozozana basi kuna hasara.

Xi Jinping ametoa kauli  hii wakati akituma ujumbe  wa pongezi kwa  ushindi wa Trump tangu rais huyo wa zamani ashinde muhula wa pili  hapo jana.

Advertisement

Trump pamoja na Kamala Harris aliyekuwa mgombea wa chama cha Democratic, wote walikuwa wameahidi kuwa na misimamo mikali dhidi ya China katika kampeni zao.

Katika kampeni zake,Trump alisema ataongeza ushuru kwa asilimia 60 kwa bidhaa zote za China zinazoingia nchini Marekani. SOMA: Huyu ndiye tajiri namba moja China

Akijibu kuhusiana na ongezeko hili la ushuru , Msemaji wa wizara wa mambo ya nje nchini China,Mao Ning amesema mivutano hii ya kibiashara kati ya nchi hizi mbili hayataweza kuleta tija katika ustawi wa maendeleo ya kiuchumi. “Hakutokuwa na mshindi katika vita vya kibiashara,’ alisema Mao.