Huyu ndiye tajiri namba moja China

CHINA: Zhong Shanshan ndiye mwanzilishi na mwenyekiti wa kampuni ya maji ya chupa ya Nongfu Spring, ambayo iliorodhesha hisa zake huko Hong Kong Septemba 2020.

Zhong mzaliwa wa Hangzhou aliacha shule ya msingi wakati wa Mapinduzi ya Utamaduni yenye machafuko huko China.

SOMA: Bezos tajiri namba moja duniani

Advertisement

Baadaye alipata kazi kama mfanyakazi wa ujenzi, mwandishi wa gazeti na wakala wa uuzaji wa vinywaji kabla ya kuanzisha biashara yake mwenyewe.

Kwa mujibu wa Forbes, utajiri wa Zhong unakadiriwa kuwa Dola bilioni 62, ambazo ni sawa na Sh trilioni 167 na bilioni 305. Mtoto wake Zhong Shu Zi ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa Nongfu.

SOMA: Tanzania yatoa wito kwa mataifa tajiri duniani