Bezos tajiri namba moja duniani

JEFF BEZOS kwa mara nyingine amechukua nafasi ya kwanza katika orodha ya matajiri duniani akimpita Elon Musk, ripoti ya Bloomberg inaeleza.

Imeripotiwa thamani ya utajiri wa bosi huyo wa Amazon ni Dola bilioni 200, akifuatiwa na Musk Dola bilioni 198.

Musk alipoteza takriban Dola bilioni 31 mwaka uliopita, wakati Bezos amepata Dola bilioni 23, kulingana na ripoti hiyo.

Advertisement

Hisa za kampuni ya Tesla ya Musk zimepungua zaidi ya 7%.

Musk alichukuwa nafasi ya kwanza mnamo Mei 2023, akimshinda Mkurugenzi Mtendaji wa LVMH (LVMHF) Bernard Arnault, ambaye anaendesha moja ya kampuni kubwa zaidi duniani na inajumuisha chapa kama vile Louis Vuitton, Dior na Celine.

Mamilionea hao watatu Musk, Arnault na Bezos wamekuwa wakishindana kila mmoja kwa nafasi ya kwanza kwa miezi kadhaa.

Mapema mwaka huu, jaji wa mahakama ya jimbo la Delaware alitupilia mbali malipo ya Musk ya 2018 yenye thamani ya zaidi ya Dola bilioni 50 ambayo yalisaidia kumfanya kuwa mmoja wa watu tajiri zaidi ulimwenguni.