USAJILI mpya wa Real Madrid kiungo wa kimataifa wa England Jude Belligham ameeleza sababu ya kuichagua jezi namba 5 huko Bernabeu.
Belligham ambaye alitambulishwa rasmi na Real Madrid amesema ni shabiki mkubwa wa gwiji wa zamani wa Real Madrid Zinadine Zidane ndio maana ameaumua kuzifuata nyayo zake.
Zidane alikuwa kivaa jezi namba 5 wakati anakipiga Real Madrid hivyo Belligham ameamua kupita kwenye nyayo za Zidane ambaye anakiri kumhusudu mno.
Kiungo huyo ambaye ni mchezaji bora wa ligi ya Ujerumani ‘ Bundesliga, msimu uliopita amejiunga na Real Madrid akitokea Borrusia Dortmund ya Ujerumani.