DAR ES SALAAM: Kocha wa Simba Abdelhak Benchikha ameondoka nchini leo kulekekea nyumbani kwao Algeria kwa ajili ya kozi ya siku tano kisha atarejea kuendelea na majukumu yake.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema makocha wasaidizi wa timu hiyo watavaa viatu vya kocha huyo kipindi atakapokosekana.
Ahmed ameongeza kuwa kocha huyo atakosekana katika michezo miwili ya timu hiyo dhidi ya Coastal Union Machi 9 na Singida Fountain Gate Fc utakaopigwa Machi 12 mwaka huu.
Benchikha ameicha Simba ikiwa nafasi ya tatu kwenye Ligi kuu baada ya kukusanya alama 36 kwenye michezo 16.