Benjamin Mkapa yaelemewa wagonjwa wa figo

DODOMA: Hospitali ya Benjamin Mkapa inakabiliwa na ongezeko kubwa la wagonjwa wa figo ambapo kwa siku watu zaidi ya 50 usafishwa damu.

Kutokana na hali hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Dk Alphonce Chandika, amewashauri wananchi kuzingatia mtindo bora wa maisha ili kulinda figo zao.

“Watu wenye tatizo la figo wanasafisha damu mara tatu kwa wiki, wananchi wanapaswa wafanye mazoezi kuzingatia mlo usioathiri moyo ili kuzilinda figo zao, ” amesema.

Advertisement

Pia, amesema wananchi wanapaswa wafanye mazoezi na kuzingatia mlo kamili usioathiri moyo ili kuzilinda figo.

Kauli ya Dk Chandika imekuja ikiwa leo ni siku ya siku ya figo duniani mwaka huu inaadhimishwa ikiwa na kauli mbiu, ‘Afya ya Figo kwa wote pamoja na upatikanaji
Bora wa matibabu.’

Aidha, amesema mpaka sasa, BMH imeshafanya oparesheni za upandikizaji figo kwa watu 36 toka huduma hiyo ianze miaka sita iliyopita.

Mwaka 2019, BMH ilikuwa Hospitali ya pili nchini kuanzisha huduma ya upandikizaji figo, lakini ndiyo Hospitali pekee kutoa huduma hiyo bila usaidizi wa Hospitali za nje.