Benki kufadhili miundombinu ya bandari Nigeria

RAIS wa Nigeria, Bola Tinubu amekutana na maofisa wa juu wa Benki ya Maendeleo ya Kiislamu (IsDB) kujadili msaada wa mabilioni ya Dola kuboresha miundombinu ya bandari na mitambo ya kuzalisha umeme.

Tinubu alifanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa IsDB, Mansur Muhtar Jumatatu huko Mecca, Saudi Arabia, msemaji wa Tinubu, Ajuri Ngelale alisema katika taarifa.

Hakutoa maelezo zaidi ya kiasi cha fedha kitakachokabidhiwa Serikali ya Nigeria.

“Tuna upungufu mkubwa wa miundombinu ya bandari, miundombinu ya umeme, na vifaa vinavyohusiana na kilimo.” Tinubu alisema katika taarifa hiyo.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x