Biden amkaribisha Trump White house

MAREKANI : RAIS  wa Marekani, Joe Biden amewataka Wamarekani kupunguza joto la kisiasa na kumaliza tofauti zao za kisiasa ili kuhakikisha mambo mengine yanaendelea.

Katika hotuba yake aliyoitoa kwenye Ikulu ya White House tangu kumalizika kwa uchaguzi, Biden amewahimiza Wamarekani kuwa na mshikamano bila kujali upande walioupigia kura katika uchaguzi wa Novemba 5.

Biden ametumia hotuba kuwataka  wanachama wa chama cha Democratic kutokata tamaa baada ya mgombea wao Kamala Harris kupoteza kinyanganyiro cha urais.

Advertisement

Kuhusu mipango ya kukabidhi madaraka kwa utawala mpya wa Trump, Biden ameahidi mchakato huo utafanyika kwa njia ya amani na desturi zilizozoeleka nchini humo.

Pia amemkaribisha Rais Mteule  Trump kwa mazungumzo Ikulu ya White house ukiwa ni utaratibu uliozoeleka kati ya rais anayeondoka na yule anayeingia madarakani.

SOMA: Trump kufutiwa mashtaka