Bil 19/- zawezesha vikundi kujiinua kiuchumi

SERIKALI imetoa zaidi ya ya Sh bilioni 19.9 kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2017 hadi 2023 kwa lengo la kuwezesha wananchi kiuchumi kupitia vikundi mbalimbali vilivyoanzishwa na wananchi.

Katibu wa Baraza la Taifa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Beng”i Issa amesema hayo leo alipokuwa mkoani Shinyanga kueleza Programu ya Uimarishaji Uchumi na Samia (IMASA).

Katibnu huyo amesema wananchi wengi hawajihusishi na taasisi za kibenki na mifumo iliyopo inatoa mikopo kwa wananchi asilimia 7 na sio kwenye mikoa yote na hiyo imekuwa changamoto huku kifungu 2;1 cha sera ya uwekezsji kinaeleza hali ya ushiriki wa wananchi shughuli za kiuchumi kuwa duni.

Mkurugenzi Uwezeshaji na Ushiriki wa Watanzania kwenye Miradi na Uwekezaji, Neema Mwakatobe amesema programu hiyo utakuwa kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Julai 2024 hadi Julai 2025 na mpaka sasa mikoa waliyotembelea wamekwisha wafikia watu 75,000 lengo kulikuwa watu 62,000 pia watafuatilia mikakati iliyokuwa imepangwa ngazi ya halmashauri na mkoa nakufahamu takwimu sahihi.

SOMA: Watakiwa kujiunga vikundi fursa za mikopo

Mshauri wa Rais Masuala ya Wanawake na Makundi Maalum kutoka Ofisi ya Rais, Sophia Mjema amesema kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi hapa nchini kilizinduliwa wilayani Kahama mkoani hapa na Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa mwaka 2017 lakini aliyekuwa akiyasimamia wakati huo ni Rais Samia Suluhu alipokuwa makamu wa Rais kipindi hicho.

“Majukwaa haya mengine yaliendelea na mengine yalikufa katika baadhi ya mikoa Ila mkoa wa Shinyanga uko vizuri na Sasa tumekuja na programu ya IMASA ambayo inataka makundi yote yashiriki na kuona Mapinduzi ya kiuchumi yanapatikana,” amesema Mjema.

SOMA: Waelimisheni wanawake wajiunge majukwaa ya uwezeshaji

Mjema amesema Mkoa wa Shinyanga niwa 16 katika kufikiwa na programu hii ambayo inawataka wananchi wawe katika mfumo nzuri wa kujiwezesha kwani tangu Uhuru mfumo haukuwa vizuri Sasa ndiyo umeanza kuboreshwa vizuri.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Annamringi Macha akifungua programu hiyo amesema wanachotaka ifikie mahali wananchi kutumia Rasilimali zao ili kujiimarisha kiuchumi ikiwa wasisitiza suala la kilimo ambapo watavuna na kusindika mazao yao ili kujiongezea kipatao.

Habari Zifananazo

Back to top button