NAIBU Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Zainabu Katimba amesema ni muhimu kwa vikundi vya vijana na wanawake kujiunga kwenye vikundi vinavyotambulika ili kuwezesha kupata fursa za mikopo na uwezeshaji unaotolewa kupitia kwwnye halmashauri nchini.
Katimba ametoa kauli hiyo alipopewa nafasi ya kusalimia katika tukio la Mwenge wa Uhuru kutembelea na kukagua kikundi cha vijana wanaojishughulisha na kazi mbalimbali za ujasiliamali kilichopo Gungu Manispaa ya Kigoma Ujiji.
SOMA: Mikopo 10% yaiva, mfumo, kanuni tayari
Naibu Waziri huyo amesema kuwa serikali ilisimamisha utoaji mikopo kwa vijana ili kuweka mazingira mazuri na wezeshi ambayo yatawezesha vijana, wanawake na makundi maalum kufikia fursa za mikopo na uwezeshaji kiuchumi zinazowekwa na serikali na kwamba vinavyoundwa zina fursa muhimu na ya haraka kufikia mikopo hiyo.
Akizungumza alipotembelea mradi huo kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru Kitaifa , Godfrey Mnzava amesema vijana wana fikra bunifu nyingi kwa ajiili ya shughuli za kiuchumi lakini wanakwamishwa na mitaji kuendeleza mawazo yao.
SOMA: Vikundi 589 bodaboda vyapatiwa mikopo
Kutokana na hilo amezitaka halmashauri kuweka mazingira wezeshi ambayo yatawezesha vijana kupata mikopo kwa ajili ya kuendesha shughuli zao za kiuchumi lakini pia kutenga maeneo ya uwekezaji ambayo vijana watayatumia kuendeshea shughuli zao za kiuchumi na kutoa mchango wao kwa Taifa.