Wizara ya ulinzi yajivunia mafanikio kwenye michezo

DODOMA; WIZARA ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), imesema inatambua vema mchango wa michezo kwa ustawi wa wanajeshi.
Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Mei 19, 2026 na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Rhimo Nyansaho akiwasilisha bungeni hotuba ya makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027.
“Hivyo, katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2025/26, Wizara imeiwezesha JWTZ kushiriki kwa mafanikio katika michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, riadha, ngumi, pool table na kuogelea.
“Naomba kulijulisha Bunge lako Tukufu japo kwa uchache baadhi ya mafanikio ambayo Wizara kupitia JWTZ imeyapata katika michezo hiyo. 28 50.
“Kwa upande wa mpira wa miguu, wizara ina timu mbili za wanaume zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara. Timu hizo ni Mashujaa FC na JKT Tanzania ambazo zinamilikiwa na JWTZ na JKT mtawalia.
“Vilevile, JWTZ ina timu nne zinazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (Championship). Timu hizo ni TMA Stars, Mbuni Football Club, Transit Camp na Gunners, ambazo zinafanya vizuri katika ligi hiyo, na ni matumaini yangu zitapanda daraja na hivyo kuongeza timu za jeshi zinazoshiriki Ligi Kuu.
“Mheshimiwa Spika, wizara ina timu mbili za mpira wa miguu wa wanawake ambazo zinashiriki katika mashindano ya ligi kuu ya kitaifa. Timu hizo ni JKT Queens na Mashujaa Queens ambazo zinamilikiwa na JKT na JWTZ mtawalia.
‘’Aidha, nina furaha kuwajulisha kuwa JKT Queens ni mabingwa wa Council for East and Central Africa Football Associations (CECAFA) kwa mwaka 2025, ilitwaa ubingwa huo baada ya kuwafunga Rayon Sports ya Rwanda katika mchezo uliofanyika tarehe 16 Septemba, 2025.

“Ushindi huu uliiwezesha timu hiyo kufuzu kuuwakilisha Ukanda wa Afrika Mashariki kwenye Klabu Bingwa ya Afrika Mwaka 2025.
“Mheshimiwa Spika, wizara katika mwaka wa Fedha 2025/26, imeshiriki katika mashindano ya Mei Mosi yaliyofanyika mkoani Njombe na kuwa mshindi wa kwanza wa jumla katika michezo mbalimbali.
Aidha, Shirika la Mzinga limeshiriki katika Mashindano ya 29 Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA), yaliyofanyika mkoani Morogoro kuanzia tarehe 25 Novemba hadi 06 Desemba, 2025 na limeweza kushika nafasi ya kwanza kwa mshindi wa jumla katika michezo hiyo,” amesema Waziri wa Ulinzi



