Bil 2.6/- kukamilisha kituo cha afya Makere

KIGOMA: KIASI cha fedha Sh bilioni 2.6 kitatumika kutekeleza mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya Makere katika kijiji cha Makere Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.
Kukamilika kwa kituo hicho kutaondoa changamoto kwa wananchi wa kata hiyo kutegemea huduma za matibabu kutoka kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyopo wilayani humo.

Meneja wa Wakala wa barabara Mkoa Kigoma, Mhandisi Chora Kimata alisema kuwa mradi huo ni sehemu ya miradi 12 ya nyongeza inayotokana na mradi mkubwa wa barabara ya kiwango cha lami ya Manyovu Wilaya ya Buhigwe hadi Kabingo Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma.
Mhandisi Kimata alisema kuwa mradi huo ambao unatekelezwa na Mkandarasi M/S Ottonde Construction & General Supplies kwa fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) umefikia asilimia 97 ya utekelezaji wake na tayari mkandarasi ameshalipwa kiasi cha Sh bilioni 1.7.

Akizungumzia kutekelezwa kwa mradi huo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Kasulu, Samuel Kadogo alisema kuwa kutekelezwa kwa mradi huo ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa kata ya Makere ambao awali msaada mkubwa wa matibabu ilikuwa kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu ambako ilibidi kuingia kwa vibali.

Akizungumza baada ya kutembelea mradi huo Mkuu wa Mkoa Kigoma, Balozi Simon Sirro alisema kuwa utekelezaji wa mradi huo ni sehemu ya mipango ya serikali kusogeza huduma kwa wananchi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo.




thisis a fantastic article, really nice created, i enjoy reading it, i will be back to check out for latest update, keep up the good work and applause. workshopmanuals.co
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com
I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com