Bil 460/- kuboresha sekta ya mifugo

SERIKALI imetenga Sh bilioni 460 kwa mwaka wa fedha 2024/25 lengo kuboresha sekta ya mifugo na kuongeza thamani ya biashara ya mifugo nje ya nchi.
Kati ya fedha hizo Sh bilioni 28.1 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mpango wa chanjo ya mifugo.
Pia madaktari wa wanyama nchini wameagizwa kutumia taaluma yao ipasavyo pamoja na kudhibiti wavamia fani hiyo ambao wamekuwa wakiuza dawa feki na kuleta athari kwa mifugo.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega alipozungumza kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kongamano la 42 la Chama cha Kitaaluma cha Madaktari wa Wanyama (TVA) jijini Arusha leo.

Amesema fedha hizo zimetengwa na serikalia kuhakikisha sekta ya mifugo inakuwa ikiwemo ongezeko la thamani ya mifugo hiyo ndani na nje ya nchi.
Amesema serikali imesikia ombi lililotolewa na viongozi wao kuhusu serikali kuajiri madaktari wasaidizi katika maeneo mbalimbali kwani waliopo hawatoshi ili waweze kutoa huduma hiyo kwenye maeneo ya vijijini na kuwa changamoto hiyo itafanyiwa kazi .

Advertisement