Bil 8.4/- kurudisha huduma meli ya MT Sangara

KIGOMA: MELI ya Mafuta ya MT Sangara iliyokuwa katika ukarabati mkubwa inatarajia kukabidhiwa kwa serikali ili kuanza kutoa huduma za kusafirisha mafuta katika nchi za ukanda wa maziwa makuu zilizomo Ziwa Tanganyika baada ya ukarabati huo kukamilika.
 
Mhandisi wa Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania MSCL ambaye ni msimamizi wa mradi wa ukarabati wa Meli ya MT Sangara, Mhandisi David Jenga amesema kuwa ukarabati mkubwa uliofanywa utawezesha ufanisi mkubwa wa utendaji kazi wa meli hiyo.
Mhandisi wa Kampuni ya huduma za meli MSCL ambaye ni msimamizi wa mradi wa ukarabati wa meli ya MT Sangara,  Mhandisi David Jenga
 
Meli hiyo yenye uwezo wa kubeba tani 380 sawa na lita 410,000 za mafuta ilisimama kufanya kazi tangu Oktoba mwaka 2020 kutokana na uchakavu wa mitambo ya injini jambo lililoathiri usafirishaji wa mafuta na hivyo serikali kutoa fedha Sh bilioni 8.4 ili kuifanyia ukarabati ambo umefikia asilimia 96%.
 
 
Kaimu Meneja wa Tawi la MSCL Kigoma, Aled Butemelo amesema kukamilika kwa meli hiyo kutatoa auheni kwa wafanya biashara wa mafuta hasa kwa nchi za Congo na Burundi ambapo meli hiyo inafanya safari zake kusafirisha mafuta.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya wataalamu wa meli kutoka Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Lukombe King’ombe amesema watatoa taarifa rasmi ya awali ili kupisha taratibu zingine ziweze kuendelea.