MAREKANI : RAIS wa zamani wa Marekani Bill Clinton amelazwa hospitalini baada ya kupata homa kali.
Kwa mujibu wa msemaji mkuu wa chama cha Demokrat Angel Urena amesema Clinton kweli alilazwa katika Kituo cha Matibabu cha Chuo Kikuu cha Georgetown huko Washington, DC siku ya Jumatatu jioni kwa ajili ya kufanyiwa vipimo na uchunguzi wa afya yake.
Hatahivyo Urena haikutoa maelezo zaidi kuhusu afya ya Rais huyo wa zamani wa Marekani ingawa ripoti za vyombo vya habari vya Marekani vinaonyesha kuwa Bill Clinton anaendelea vizuri na matibabu.
SOMA: Trump kulipa Dola milioni 350, afungiwa biashara miaka mitatu