Bima ya afya kwa wote mpango mzima – Dk Molel

DODOMA: Serikali imetoa wito kwa Watanzania, Viongozi wa kisiasa, kidini na kimila kuungana na Serikali katika kuhamasisha umma kujiunga na Bima ya Afya kwa wote pale mchakato utakapoanza rasmi.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel wakati akijibu swali la Mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba aliyetaka kujua kauli ya Serikali juu ya Bima ya Afya kwa Watoto.

Dk. Mollel akijibu swali hilo amesema kuwa nchini kuna watoto milioni 31, milioni 1.

5 wako kwenye mfumo wa bima ya afya ya sasa na milioni 30.7 wako kwenye mifumo ya bima za afya nyingine zilizopo nchini.

“Niwahakikishie wananchi kuwa ujio wa bima ya afya kwa wote utakuwa suluhisho la changamoto ya matibabu kwa wananchi wote bila kujali hali ya kiuchumi na kikwazo cha fedha, hivyo naomba mchakato utakapoanza wananchi mjitokeze kujiunga na skimu zitakazobainishwa ambazo zitakua kwa rika zote,”amesema  Mollel.

Habari Zifananazo

Back to top button