“NDOTO yangu ya kuwa daktari imetokana na matakwa pamoja na dhamira ya kusaidia wagonjwa. Mimi na wazazi wangu tulipata shida sana katika mambo ya tiba hivyo nilitamani kuwa daktari kusaidia jamii.
Haya ni maneno ya Profesa Karim Manji, mshindi wa tuzo ya Alumni Award of Merit kutoka Shule ya Afya ya Chuo Kikuu cha Harvard (Harvard T.H. Chan School of Public Health). Profesa Manji amezaliwa Juni, 1959 mkoani Tabora. Wazazi wake pia wamezaliwa Tanzania na kubahatika kupata watoto 11.
Profesa huyu ambaye ameipai[1]sha Tanzania na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhim[1]bili (MUHAS) kimataifa, alihitimu masomo yake ya awali katika Shule ya Msingi Muhimbili mwaka 1972. Baada ya hapo alijiunga na Shule ya Sekondari Forodhani (1976) ndipo aliteuliwa kujiunga na Shule ya Sekondari Pugu kwa ajili ya ma[1]somo ya Kidato cha Tano na Sita.
“Sikufanikiwa kumaliza maso[1]mo yangu ya kidato cha sita kwani niliugua mno. Hata hivyo, wazazi wangu walifariki nikiwa kijana mdogo,” anasema Profesa Manji. Profesa Manji ambaye ni Mkufunzi na Mtafiti wa Muhas, anasema baada ya kuugua, kabla ya kuendelea na masomo, alifanya kazi ya ukarani kwa miaka mitatu. Anasema kupitia kwa mfadhili na walezi wake aliowatambulisha kwa jina la Anver na mama Keki, alikwenda India kwa ajili ya ma[1]somo ya kidato cha tano na sita.
“Nilifanikiwa kupata nafasi kupitia uteuzi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuchaguliwa kusoma Udaktari wa Tiba. Mwaka 1980 nilianza kusoma udaktari katika Chuo cha MKCG College, Berhampur, Orissa na baada ya kumaliza mafunzo kwa vitendo (internship) nilifanya kazi kwa muda mfupi New Delhi na hatimaye kurudi nyumbani,” anasisitiza.
Profesa Manji ana mke na watoto wanne ambao ni Zainab, Hussen, Ummu na Siraaj. Watoto wake wanne wamefuata nyayo zake kwa namna tofauti. Zainab ni mkufunzi katika Shule ya Uuguzi Muhas, Hussen ni dak[1]tari bingwa wa wagonjwa mahu[1]tuti na Dharura Aga Khan, Ummu anajihusisha na bioteknolojia huko Ujerumani na Siraaj anafanya kazi katika sekta ya fedha kimataifa.
Mke wa Profesa Manji ni Kiongozi wa Shule ya Msingi ya Bilal Comprehensive School, Tandika Dar es Salaam kwa miaka 22 sasa. Profesa Manji anasema kilichomsukuma kuwa daktari bingwa wa watoto ni mwalimu wake katika Chuo cha Berhampur.
Anasema mwalimu huyo alikuwa katika idara ya watoto na kwamba alikuwa mkarimu mno na kila alipotibu mtoto na kum[1]wezesha kupona, alijisikia furaha iliyoonesha mafanikio na faraja. “Nilikuwa nawaza, upendo na ukarimu na nionapo watoto wanavyotabasamu na kufurahi wanapopata tiba na kuruhusiwa, inaleta amani na faraja,” anasema.
Pia, anasema kuwa sababu ny[1]ingine iliyomfanya asomee udaktari bingwa wa watoto, ni baada ya kushuhudia kwamba watoto husu[1]sani wachanga wanapoteza maisha kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uhaba wa madaktari. Profesa Manji ambaye amean[1]dika machapisho zaidi ya 360 ya utafiti mbalimbali eneo la afya ya watoto, anasema kuna sababu kadhaa zinazochangia wazazi kutotekeleza majukumu yao na watoto kutopata huduma stahili.
Anasema kuwa wazazi hawafa[1]hamu dalili mbalimbali za magon[1]jwa kwa watoto. Kwa mfano, mtoto kupumua kwa haraka inaashiria Nimonia wakati mzazi anafikiria kwamba labda amechoka au ana mafua. Katika lishe, anasema mara yingi eneo hilo lina sintofahamu kuhusu umuhimu wa lishe. “Mtoto anahitaji wanga kidogo na protini nyingi.
Sisi tunawaza kwamba akimaliza sahani nzima ya wali (ubwabwa) na rojo kidogo la maharage tunadhani kwamba mtoto ameshiba,” anasema na kuongeza: “Kitendo hicho kinampa mtoto wanga zaidi na protini finyu, inat[1]akiwa alishwe kibakuli kizima cha maharage na wali kidogo kama kiganja.
” Kuhusu magonjwa ya watoto ambayo hayapewi kipaumbele, Profesa Manji anasema changa[1]moto za utapiamlo kwa watoto wachanga hususani wale chini ya mwaka mmoja bado inahitaji jitihada za dhati kukabiliana nalo. Anasema licha ya serikali kufanya mipango ya makusudi kuboresha afya ya watoto wachanga, lishe kwa watoto ni muhimu. Miongoni mwa maeneo ambayo Profesa Manji aliyafanyia kazi ni kuokoa maisha ya watoto wachanga wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti).
Anasema zipo sababu mbalim[1]bali huchangia watoto kuzaliwa kabla ya wakati ikiwemo mama mwenye umri mdogo ambaye hajafika kilele cha ukuaji (Adolescent girls). Sababu nyingine ni mama mwe[1]nye uzito mdogo na mwenye kimo kifupi, kuzaa mara kwa mara yaani (frequent pregnancies) kila mwaka anajifungua.
“Utapiamlo wa mama, upun[1]gufu wa damu kwa mama, maam[1]bukizo ya magonjwa mbalimbali pamoja na kupata mapacha au zaidi,” anaeleza. Anafafanua kuwa “Sina hesabu ni watoto wangapi njiti ambao nimewasaidia na kuokoa maisha yao lakini unapokuwa mwalimu, unajua kwamba kila daktari uliyemfundisha ataokoa maisha.
Na hiyo ndio ninajivunia. Lakini pamoja na kufanya utafiti ambao unalenga kuboresha afya ya mtoto.” Akizungumzia tuzo ya Chuo cha Harvard aliyoipata, Profesa Manji anasema tuzo hiyo ni ya kuthaminiwa licha ya kwamba haina malipo ya kifedha lakini jinsi inavyotolewa ni kwa kupitia mambo uliyofanya katika kusaidia afya ya jamii. “Ni tuzo yenye sifa kubwa na yenye kujulikana duniani. Kwa tuzo hii ni ahadi na heshima, nitajaribu kadiri ya uwezo wangu kuweka hadhi hiyo,” anasema.
Vilevile anaeleza kuwa kwa tuzo kama hiyo, dunia nzima inatambua mchango wake hivyo kunapotokea fursa ya utafiti, anatafutwa kuendesha na kwamba inajenga hadhi ya Chuo cha Muhas na taifa kwa ujumla. Mkufunzi huyo wa Muhas anasema kuwa wapo wanafunzi wengi wanaosomea udaktari na wenye kutamani kufikia ndoto kama zake, wasichoke na pale wa[1]napoona changamoto wanapaswa kukabiliana nazo na kamwe wasirudi nyuma kuitumikia jamii na Mungu atawatukuza. Anasema sekta ya afya inafanya vizuri nchini tofauti na alivyoiona miaka 35 nyuma.
“Sekta ya afya ilivyo sasa na miaka mitano nyuma ni tofauti sana na ni dhahiri tumepiga hatua. Hata hivyo, bado inatakiwa kufanya kazi kubwa na kuweka mikakati ya makusudi ya kubore[1]sha afya ya watoto wachanga,” anasema Profesa Manji.
Tuzo nyingine alizochukua Profesa Manji ni ya Aprili 2019 na Mei 2023 ya Publication in High Impact Journal kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Tuzo ya Excellence in Patient Care iliyotolewa na Royal College Physicians London, Uingereza mwaka 2019. Novemba mwaka 2017 alipata tuzo ya Fellow of Royal College of Paediatrics and Child Health Lon don na Julai mwaka huohuo, alipata tuzo ya Fellowship Royal College of Pediatrics and Child Health. Profesa huyo ametoa huduma na kusaidia watoto wachanga kwa zaidi ya miaka 20. Alifanya utafiti kuhusu kuzuia maam[1]bukizi ya Virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Katika utafiti huo ulichangia kubadilishwa kwa sera kuhusu kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT). Majaribio ya kuzuia maambukizo hayo yalifanywa pia kwa wanawake ambao wa[1]likuwa wananyonyesha uliojulikana kama Myths and Realities of Breast Feeding and HIV in Africa.
Hakuishia hapo, Profesa Manji pia alifanya utafiti kuhusu ugonjwa wa usonji ambao huwapata watoto kutokana na ku[1]tokuwepo kwa uelewa kuhusu matunzo ya watoto wenye ugonjwa huo Tanzania. Aliwasimamia watahiniwa wa Shahada ya Uzamivu wa Chuo Kikuu Huria cha Uingereza, kufanya utafiti kuhusu usonji Tanzania na kuchangia mabadiliko katika sera na kuongeza uelewa wa ugonjwa huo.
Tafiti nyingine alizofanya ni Neurode[1]velopmental Assessments, Lishe na Afya ya Mtoto na miongoni mwa tafiti zinazo[1]endelea ni kuhusu Low Birth Weight Infant Feeding Exploration (LIFE!) unaofadhiliwa na Harvard TH Chan SPH, BMGF.
Pia kuna utafiti kuhusu Possible Serious Bacterial Infection in Newborn (uwepo wa maambukizi ya bakteria kwa watoto wachanga) ulioanza Aprili, 2021. Baada ya kutolewa kwa tuzo hiyo, Rais Samia Suluhu Hassan alimpongeza Profesa Manji kwamba ni Bingwa, Mkufunzi na Mtafiti katika eneo la tiba ya watoto na afya ya vijana.
“Kwa zaidi ya miaka 30, amekuwa daktari, mkufunzi na mtumishi wa kupigiwa mfano katika Hospitali ya Taifa na Chuo Kikuu cha Afya na Tiba Shirikishi, Muhim[1]bili. Tunajivunia kujitoa kwako kwa nchi yetu, utafiti, ushauri, utumishi na malezi yako kwa mamia ya wanafunzi ambao sasa ni madaktari katika eneo hili muhimu la afya kwa nchi yetu,” aliandika Rais Samia. Profesa Manji ni mfano wa utumishi uliotukuka, mtu ambaye ndoto yake ya kusaidia wagonjwa imebadilisha maisha ya maelfu, si tu nchini Tanzania bali ulimwenguni kote.