Rais Samia afanya uhamisho wa viongozi

DAR ES SALAAM; RAIS wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bakari Machumu, ikinukuu taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Moses Kusiluka, imesema, Rais Samia amemteua Dk Eveline Munisi kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, akichukua nafasi ya Rahma Riyadh Kisuo, ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Pia taarifa imesema Eliakim Maswi amehamishwa kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, kwenda kuwa Katibu Muuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalumu, wakati Dk John Jingu amehamishwa kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalumu kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button