Binti wa Mchambuzi wa maswala ya Kisiasa nchini Urusi ameuawa kwa bomu lililotegwa ndani ya gari nje kidogo ya jiji la Moscow, kamati ya uchunguzi imesema.
Darya Dugina, ambaye babake ni mchambuzi wa kisiasa wa Urusi Alexander Dugin, alifariki wakati Toyota Land Cruiser aliyokuwa akiendesha ilipopasuliwa na mlipuko mkubwa kijiji cha Bolshiye Vyazemy km 20 magharibi mwa mji mkuu. Timu ya uchunguzi imesema tukio hilo limetokea mwendo wa saa 3.30 asubuhi kwa saa za Urusi.
Walioshuhudia walisema vifusi vilitupwa barabarani huku gari hilo likiteketea kwa moto kabla ya kuangukia uzio.
“Kifaa cha vilipuzi kinachodaiwa kuwekwa kwenye gari la Toyota Land Cruiser kililipuka kwa mwendo wa kasi kwenye barabara kuu ya umma, na kisha gari hilo kushika moto,” wachunguzi waliandika katika ripoti yao ya tukio hilo.
Dereva wa kike alifariki papo hapo. Utambuzi wa marehemu umeabaini ni mwandishi wa habari na mwanasayansi wa siasa Darya Dugina.