BITEKO: Kinyerezi itazalisha umeme hadi megawati 1,000

DAR ES SALAAM: NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk Doto Biteko amesema serikali inatarajiwa kuongeza uwezo wa kituo cha kuzalisha umeme kwa njia ya gesi cha Kinyerezi kutoka megawati 600 hadi kufikia 1000 ili kuongeza upatikanaji wa umeme.
Biteko ameyasema leo hayo alipotembelea mradi wa kuzalishia umeme wa Kinyerezi l na ll ambavyo vinazalisha jumla ya megawati 600 ili kuzalisha megawati 1000 ikifuatia ongezeko la matumizi ya nishati.
Aidha, Biteko amesema mchango wa sekta ya nishati umepanda hadi kufikoa asilimia 14 na kuwa sekta ya pili inayokua na kuchangia katika pato la taifa huku akisisitiza watanzania kuendelea kulinda miundombinu ya nishati wakati serikali ikiwa inaendelea kuwekeza katika wizara hiyo.

Naye, Mkurugenzi wa Shirika la Umeme (TANESCO), Lazaro Twange pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo wameishukuru serikali kutokana na uwekezaji ilioufanya katika sekta ya nishati huku wakieleza umuhimu wa ziara ya viongozi katika miradi ya nishati ya umeme.
SOMA ZAIDI
Katika ziara yake Naibu Waziri Mkuu, Doto Biteko amekagua miundombinu ya uzalishaji wa umeme ya kinyerezi pa moja na kituo cha kupokea gesi kutoka mtwara kabla ya kuelekea katika vituo vya kinyerezi l na ll.



