GEITA;NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko alisema miezi michache iliyopita, tatizo la mgawo wa umeme lilikuwa likimkosesha amani.
Alisema kwa juhudi za viongozi wakuu wa serikali, Wizara ya Nishati na Shirika la Umeme Tanzania(Tanesco), tatizo limefikia tamati. Dk Biteko alisema kwa sasa nchi ina umeme wa kutosha kuwezesha Watanzania kufanya shughuli zao za kiuchumi.
Isome pia:https://habarileo.co.tz/dk-biteko-aitaka-tanesco-kumaliza-kero-ya-umeme/
Alisema hayo jana kwenye ibada alipoungana na waumini wa Kanisa la AIC Ushirombo wilayani Bukombe mkoani Geita.
“Nashukuru Rais Samia Suluhu Hassan ameweka mipango madhubuti kwenye sekta yetu ya nishati ambayo sasa imefanya tuwe na umeme wa kutosha na hatuna mgawo wa umeme,” alisema.
Isome pia:https://habarileo.co.tz/dk-biteko-avunja-bodi-kampuni-ya-tanesco/
Kutokana na uwapo wa umeme mwingi wa kutosha, Dk Biteko amewataka Watanzania kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo.
Alisema serikali inaendelea kuhakikisha inaweka mazingira wezeshi ya kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi.