Blinken na Hakan waamua kusitisha mapigano Gaza
UTURUKI : WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan na mwenzake wa Marekani, Antony Blinken wamejadiliana kuhusu juhudi mpya za kutafuta makubaliano ya kusitisha mapigano huko Gaza, kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Uturuki, Oncu Keceli amesema Fidan na Blinken wamejadiliana kuhusu maendeleo ya kikanda.
Wakati huo huo, kundi la Hezbollah la nchini Lebanon leo limerusha zaidi ya roketi 50, na kushambulia nyumba kadhaa binafsi katika Milima ya Golan inayokaliwa na Israel.
Shambulizi hilo limefanyika siku moja baada ya Blinken kukutana na wapatanishi wa Misri na Qatar, wakati akiendeleza juhudi za kidiplomasia kuhakikisha vita huko Gaza vinasitishwa.
SOMA : Idadi ya waliouawa Gaza sasa zaidi ya 40,000
Hatahivyo jeshi la Israel limefanya mashambulizi ya mabomu katika maghala ya kuhifadhia silaha ya Hezbollah kwenye Bonde la Bekaa nchini Lebanon.