Idadi ya waliouawa Gaza sasa zaidi ya 40,000

IDADI ya wapalestina waliouawa kutokana na vita kati ya jeshi la Israel na kikundi cha Hamas cha Palestina katika Ukanda wa Gaza tangu Oktoba 7, 2023 imefikia 40,005, imesema wizara ya afya ya Hamas.

Idadi hiyo iliyofikia leo ni sawa na asilimia 1.7 ya watu milioni 2.3 wa eneo la Gaza.

SOMA: Papa asikitishwa na vita Gaza, asema silaha hazileti amani

Pamoja na vifo hivyo, karibu asilimia 60 ya majengo katika eneo la Gaza yameathiriwa au kuharibiwa tangu kuanza kwa vita.

Hata hivyo takwimu hizo za Wizara ya Afya Gaza za watu waliouawa hazijatofautisha kati ya raia na wapiganaji.

 

Idadi ya waliouawa upande wa Israel inakadiriwa kuwa 1,410, wakiwemo wanajeshi 395 huku 1,139 wakiuawa katika mashambulio ya Oktoba 7.

Vita inayoendelea kati ya jeshi la Israel na wapiganaji wa Hamas ilianza baada ya vikundi vya wapalestina kuvamia kusini mwa Israel.

Habari Zifananazo

Back to top button