DAR-ES-SALAAM: Msarifu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Taasisi ya Benjamin William Mkapa itaendelea kuunga mkono juhudi za serikali kwa kuchangia kuandaa nguvu kazi, kuwaendeleza na kuboresha mifumo kupitia programu ya Mkapa Fellows katika sekta ya afya.
Dkt.Mwinyi ameyasema hayo wakati wa kumbukizi ya tatu ya Hayati Benjamin William Mkapa katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Aidha Rais Dkt.Mwinyi ameleeza kuwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatarajia kujenga Hospitali ya Rufaa ya Binguni itakayokuwa na vitanda 600 hivi karibuni.
Halikadhalika, Rais Dkt.Mwinyi amesema SMZ imetoa ajira mpya 1,050 za watumishi wa afya, imejenga jumla ya nyumba 80,16 kila wilaya zilizogharimu shilingi bilioni 20 ili kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi wa sekta ya afya na kuwapa motisha ya kazi.
Vilevile Rais Dkt.Mwinyi amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa juhudi anazochukua za kuboresha sekta ya afya nchini.

SOMA: Benjamin Mkapa kuongeza wigo tiba nguvu za kiume