Bodi TGDC yatembelea miradi ya kimkakati Mbeya, Songwe

BODI ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi nchini (TGDC), imekamilisha ziara ya siku tatu kutembelea miradi ya kimkakati inayotekelezwa na kampuni hiyo  Mikoa ya Mbeya na Songwe.

Bodi hiyo iliyozinduliwa Julai mwaka huu, ilifanya  ziara yake ya kwanza na kujionea maendeleo ya miradi ya jotoradhi, ambayo ni chanzo adhimu cha nishati ya uhakika, endelevu na rafiki wa mazingira.

Ziara hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi Prof. Shubi  Kaijage, ambaye alisema amefarijika na maendeleo na jitihada zinazoendelea katika miradi ya jotoardhi na kwamba wanaendelea kuishauri na kuielekeza menejimenti ya TGDC, ili ifikie malengo ya megawati 200 ifikapo mwaka 2025, kama mipango mikakati ya kampuni ilivyoainishwa  na kutimiza malengo ya serikali.

Kwa upande wa Kaimu Meneja Mkuu wa TGDC, Mhandisi Shakiru Idrissa wakati wa ziara hiyo, alisema kazi ya kuchoronga visima vya jotoardhi itafanyika kwa kipindi cha miezi minne hadi sita kwa upande wa mradi wa Ngozi baada ya kufika mtambo wa kuchoronga (drilling rig), unaotazamiwa kufika mwishoni mwezi ujao.

Alisema kampuni inategemea kupata megawati 70 za awali kwa vipindi vya awamu mbili, awamu ya kwanza megati 30 na ya pili megawati 40 ifikapo mwaka 2025.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x