Bodi ya Wakurugenzi Self watembelea wanufaika

Watoa elimu ya ujasiriamali, wataka watanzania kuchangamkia fursa

BODI  ya Wakurugenzi wa Mfuko wa fedha wa SELF ulio chini ya Wizara ya fedha imewatembelea wanufaika wake waliopo Zanzibar kwa lengo la kuainisha fursa mbalimbali za kifedha zinazotolewa na mfuko huo hapa nchini.

Wanufaika wanaolengwa na mfuko huo ni wajasiriamali, wafanyabisahara, wanaohitaji kuboresha makazi pamoja na taasisi za fedha.

Meneja Masoko na Uhamasishaji wa mfuko wa SELF Microfinance, Linda Mshana akizungumza amesema mfuko huo umelenga kukidhi mahitaji ya mikopo kwa makundi mbalimbali Tanzania bara na visiwani.

Ziara ya uongozi wa SELF imekuja wakati huu ambapo mahitaji ya mikopo kwa nchi zinazoendelea yanatajwa kuwa hitaji la msingi katika kukuza ujasiriamali, biashara, Kilimo na Ufugaji vilevile hata kupata makazi na kuwekeza kwenye viwanda.

Linda amesema, kulingana na mahitaji na mkopo na kuongezeka kwa utitiri wa taasisi za mikopo, vijana wa kitanzania wanashauriwa kuungana na kukopa kwenye taasisi za fedha za kuaminika na zenye usimamizi wa serikali ili kuepuka fedhea katika mikopo hiyo.

“Tunawashauri pia kutumia mikopo hiyo ya fedha  kwa ufanisi kwa kuanzisha  miradi ya kimkakati ambayo imezingatia tafiti za kutosha na ushauri elekezi kutoka kwa wabobezi wa masuala ya kifedha ili mikopo hiyo iwe na manufaa ya familia zao na taifa kwa ujumla.”Amesema

Nae, Meneja wa mfuko wa SELF Zanzibar Ramadhani Masebu anazitaja changamoto kubwa mbili ambazo zinaweza wakwamisha wakopaji hasa hapa nchin kutokana na  changamoto ya mitaji.

Amezitaja changamoto hizo ni elimu ya mikopo na elimu ya biashara kuwa ndio huathiri  marejesho na kuua biashara za watu wengi.

“Kwa kutambua changamoto hiyo tumeamua kutoa elimu na kuzifikia wilaya zote za Zanziba ili wateja wetu waweze kupatiwa elimu itakayowasaidia kutimiza malengo ya wakopaji.” Amesema Masebu  na kuongeza

“Katika kuwafikia wajasiriamali wetu wadogo na wa kati, tunajitahidi sana katika kutoa elimu ya mikopo na elimu ya biashara na hili ni eneo muhimu sana tunaita “Capacity Building”; …… “ ni eneo zuri sana, tumeona tunapotoa mikopo ni lazima tutoe na elimu ya ujasirimali na mikopo kwa manufaa ya watu wetu, lengo letu ni kuhakikisha tunawahudumia wajasirimali wote, wadogo, wa kati na hata wakubwa” amesisitiza

Masebu anasema zipo aina nane za mikopo ambazo zinatolewa na mfuko wa SELF Microfinance ambazo ni mkopo wa Kilimo,Biashara, Makazi,Mshahara, mkopo wa Pamoja, mkopo wa Imarika, Mkopo wa Mahitaji na Mkopo wa Mkulima.

Kwa upande wa Linda ameongezea kwa kusema kuwa  nia ya mfuko huo ni kuendela kuwapatia watanzania elimu na kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo hapa nchini.

“Kila mtanzania ana fursa kubwa ya kupata mkopo na kujikuza kiuchumi, kwa wajasiriamali wote wa chini, wa kati, wakubwa, wafanyakazi, na watu wanaotaka kuboresha makazi.

“Wale waliopo kwenye vikundi wanaotaka mikopo ya kujiinua kiuchumi, wasiache fursa zikakupita, tuna wafanyakazi waliokidhi na wana weledi wa kuhudumia wajasirimali wote wanaotaka kujiinua kichumi.” amesema.

 Je, wapi Marafiki zetu hutushawishi kukopa?

Zipo taarifa kem kem za wakopeshaji na marafiki, ndugu na jamaa ndiyo kwa kiwango kikubwa washauri au wadhamini wa kwanza wa wapi tukakope.

Miongoni mwa wanufaika wa mkopo ni pamoja na wasimamizi na wamiliki wa shule ya Bright Future Academy ya Zanzibar na Mwalimu Ibrahimu Julius ambaye ni Mkuu wa shule hiyo iliyopo Mkoa wa Mjini Magharibi anasema baada ya kupata taarifa kutoka kwa marafiki waliona manufaa yake.

“Tulinufaika na mkopo huu wa SELF kwani tulikabiliwa na uhaba wa madarasa kwa kiwango kikubwa, tuliweza kukopa na kuongeza vyumba vya madarasa 17 na kufanya ongezeko la madarsa kutoka 14 hadi 31 na kwakweli tunayaona manufaa na mkopo,”amesema na kuongeza

“Kabla ya kukopa tulikuwa na hofu ya kukopa na kwa kweli hatukuwahi kukopa sehemu nyingine yoyote, ila wataalamu wa SELF walitupa elimu na wakatueleza urahisi wa marejesho endapo utapata mkopo kutoka kwenye mfuko huo na mapaka sasa tunajivunia Bright Future ni shule yenye madarasa ya kutosha” amesema Julius.

Changamoto zinazowazonga wakopaji

Zipo changamoto lukuki zinazoripotiwa mara kwa mara kwenye vyombo vya habari kutotii kiu ya wanaohitaji kwa wakati muafaka.

Dora Mathias Baliza ambaye ni mmiliki wa Bright Future Academy ya Zanzibar anasema baadhi ya taasisi nyingi zimekuwa hazikidhi mahitaji ya mikopo ya wahitaji kwa wakati jambo ambalo linakatisha tamaa.

“Ni Mungu tu kwa sababu, binafsi nilikuwa sifahamu kuhusu hii taasisi ya SELF kwani benki moja walikuwa na fomu zangu na hawakunipa majibu kwa muda mrefu na nilikuwa naonekana kama sikopesheki, na nilikuwa kama nakata tamaa” amesema Dora

Akifafanua anasema “siku moja wakati napita maeneo ya Posta nikaona mabango na kikaamua kufuatilia, na ndipo nikakutana na mfuko huu wa SELF, nilipojaribu kwa kweli Mungu alitenda na ule mkopo wenu wa kwanza kwakweli ulituvusha katika mazingira ambayo tulikuwa tumekata tamaa” alisema Dora.

Alisema,  mpaka sasa shule yake imekuwa ya mfano na wanafikiria kuendelea kuboresha mazingira ya shule na wamefika hapo kwa sababu ya mchango mkubwa wa mfuko huo wa Serikali na hadi sasa wana uwezo wa kukopa viwango vikubwa na wanamudu marejesho na hata baadhi ya benki sasa wanawafuata ili wakope kwao.

“Jambo la msingi kwa wakopaji ni kuweka mahesabu vizuri ili uwe na uwezo wa kukopa na kurejesha kadri ya makubaliano na hilo ndilo litaleta manufaa na kukuza biashara na uweze kukopesheka zaidi.” Amesisitiza Dora

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
8 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
yirzoharde
yirzoharde
1 month ago

My first payment is $27,000. I’m thrilled since this is the first time I’ve truly earned stuff. From this point on, I’m going to work even harder, and I can’t wait till the next vs10 week to get paid. Click the home tab to find out more.
.
.
Using Here————————————>> https://fastinccome.blogspot.com/

Shawn
Shawn
Reply to  yirzoharde
1 month ago

I am making over $30k a month working part time. I am a full time college student and just working for 3 to 4 hrs a day. Everybody must try this home online job now by just use this Following Website…….. https://www.Worksprofit.com

Last edited 1 month ago by Shawn
MAPINDUZI YA ELIMU
MAPINDUZI YA ELIMU
Reply to  yirzoharde
1 month ago

WAZO JADIDIFU UKIONA WEKAZO HAWAFANYI KAZI KAMA RAIS WA TANZANIA (HAFANYI KAZI VIZURI KABISA) NA UNATAKIWA UPINDUE NCHI UTATUMIA CHOMBO GANI CHA HABARI… MAPINDUZI YA KIJESHI MATHARANI KUTAKUA NA RAIS AJAE KAMA MKAPA HUKO
·        THE GUARDIAN,
·         THE CITIZEN,
·         MWANANCHI,
·         DAILY NEWS,
·        NIPASHE,
·        TBC TAIFA,
·         RFA,
·        RADIO ONE,
·        CLOUDS FM,
·        TBC1,
·        ITV, NA
·        AZAM TV.

LisaWright
LisaWright
1 month ago

Single Mom With 4 Kids Lost Her Job But Was Able To Stay On Top By Banking Continuously DOLLER 1500 Per Week With An Online Work She Found Over The Internet… 

Check The Details HERE…..  https://webonline76.blogspot.com/

Last edited 1 month ago by LisaWright
MAPINDUZI YA ELIMU
MAPINDUZI YA ELIMU
Reply to  LisaWright
1 month ago

WAZO JADIDIFU UKIONA WEKAZO HAWAFANYI KAZI KAMA RAIS WA TANZANIA (HAFANYI KAZI VIZURI KABISA) NA UNATAKIWA UPINDUE NCHI UTATUMIA CHOMBO GANI CHA HABARI… MAPINDUZI YA KIJESHI MATHARANI KUTAKUA NA RAIS AJAE KAMA MKAPA HUKO
·        THE GUARDIAN,
·         THE CITIZEN,
·         MWANANCHI,
·         DAILY NEWS,
·        NIPASHE,
·        TBC TAIFA,
·         RFA,
·        RADIO ONE,
·        CLOUDS FM,
·        TBC1,
·        ITV, NA
·        AZAM TV.

JuliaDeni
JuliaDeni
1 month ago

Earn money by just working online. You are free to work from home anytime you choose. You may earn more than $600 per day online by working only 5 hours every day. In my leisure time, I made $18,000 from this.
.
.
Detail Here—————————————————>>>  http://Www.OnlineCash1.Com

EverestAbilene
EverestAbilene
1 month ago

My buddy’s mother makes $90 per hour working on the computer (Personal Computer). 6r9 She hasn’t had a job for a long, yet this month she earned $15,500 by working just on her computer for 9 hours every day.
Read this article for more details…………..>  http://www.SmartCash1.com

MAPINDUZI YA ELIMU
MAPINDUZI YA ELIMU
1 month ago

WAZO JADIDIFU UKIONA WEKAZO HAWAFANYI KAZI KAMA RAIS WA TANZANIA (HAFANYI KAZI VIZURI KABISA) NA UNATAKIWA UPINDUE NCHI UTATUMIA CHOMBO GANI CHA HABARI… MAPINDUZI YA KIJESHI MATHARANI KUTAKUA NA RAIS AJAE KAMA MKAPA HUKO
·        THE GUARDIAN,
·         THE CITIZEN,
·         MWANANCHI,
·         DAILY NEWS,
·        NIPASHE,
·        TBC TAIFA,
·         RFA,
·        RADIO ONE,
·        CLOUDS FM,
·        TBC1,
·        ITV, NA
·        AZAM TV.

Back to top button
8
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x