BENKI Kuu Tanzania (BOT) inaendelea kuchukua hatua mbali mbali ili kushusha riba hadi asilimia 9 .
Hayo yamesema na Gavana wa BOT benki hiyo Profesa Florens Luoga kwenye kongamano la uwasilishaji wa machapisho ya wataalam wa fedha kuelekea mahafali ya kwanza ya Chuo cha Benki Kuu Tanzania yanayotarajiwa kufanyika Ijumaa ya Novemba 25, 2022.
Amesema hadi sasa benki nchini zinatoa mkopo kwa riba ya kati ya asilimia 11 na 13.
“BoT tumepunguza gharama za uendeshaji wa benki nchini kutoka asilimia 70 hadi 50 na kuanzisha mfuko maalum wa kukopesha mabenki kwa sharti la kukopesha fedha kwa watu kwa riba isiyozidi asilimia 10.” Amesema Luoga
Amesema lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha wanafikia riba ya dijiti moja.
Profesa Luoga, pia amezitaka benki zote zinazokopesha katika shughuli za kilimo ziwe zinafuatilia maendeleo ya miradi hiyo.
Amesema wananchi wa Tanzania zaidi ya asilimia 90 ni wakulima na au wanafanya shughuli ndogo ndogo za biashara
Aidha, amesema thamani ya fedha ya Tanzania inaendelea kubakia katika hali ya utulivu kwa hatua thabiti haswa wakati huu nchi inapopitia changamoto za uviko-19 na changamoto za vita za Urusi na Ukraine.
Amesema chuo cha benki kuu na kushirikiana na vyuo vingine wataendeleza juhudi katika kufanya utafiti wa usimamizi wa fedha.