BOT kuwakwamua waathirika mikopo umiza, kausha damu

DAR ES SALAAM: BENKI Kuu  ya Tanzania (BOT) imezindua rasmi mtaala wa wakufunzi wa elimu ya fedha nje ya mfumo rasmi ambapo wananchi watapata elimu ya matumizi sahihi ya fedha ikiwemo akiba  ili kuepuka mikopo umiza  na kausha damu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo leo jijini Dar es Salaam, Gavana wa BOT, Emanuel Tutuba amesema mtaala huo utakuwa na fursa nzuri ya kuona matokeo chanya katika shughuli mbalimbali kwenye upatikanaji wa mikopo, matumizi na hata urejeshaji kwa makundi ya wajasiriamali, wakulima, wavuvi na wengine.

Advertisement

 

Amesema wanafahamu  changamoto ya mikopo chechefu inayotokana na kutokuwa elimu stahiki ya utaalamu wa fedha  hivyo wanaendelee kushirikia wote ili kutoa elimu.

 

“Utakuta mtu  anaweza kukopa ili kufanya shughuli ambazo haziwezi kurejesha ukopo huo sio mzuri  hii yote ni elimu duni ya fedha na wengine wanamipango mingi akipata fedha ni mwepesi kubadili vipaumbele kitu ambacho sio sahihi,” amesema Gavana.

 

Tutuba amesema kuwa kila mmoja ana uwezo wa kushika fedha shida inakuja namna ya kuzitawala ambapo watu  wanakuwa na matumizi mabaya hivyo mtaala huo utawawezesha kutoa elimu ili iwafikie wananchi.

“Watu tunawasisitiza kabla ya kuchukua mikopo lazima awe amefahamu masharti kwamba unapoingia mkataba lazima wote mridhie tunasisitiza mikopo yote watu lazima wakubaliane  na mtu akiambiwa riba afahamu ni ya mwaka,mwezi,siku maana kuna wengine wanachukua mkopo anazidisha wiki mbili atarejesha na ataambiwa kuwa  atalipa faini.

 

Wadau watatoa elimu hiyo ya fedha mwaka 2024 nchi nzima ambapo  wakufunzi mbalimbali wakiwemo wale wenye elimu ya fedha,wanaotoka vyuo mbalimbali,halmashauri,taaluma zingine  watapata mafunzo ya wiki mbili na kupewa vyeti.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *