BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imezifungia programu tumizi 69 zilizokuwa zikitumika kutoa mikopo kidijiti. Gavana wa BoT, Emmanuel Tutuba ameeleza kuwa wamebaini kuna ma jukwaa na programu tumizi yanayo jihusisha na utoaji wa mikopo kidijiti bila ya kuwa na leseni na idhini kutoka BoT.
Tutuba alieleza kuwa programu hizo 69 hazina kibali na haziruhusiwi kuendelea na shughuli za utoaji mikopo kidijiti.
Taarifa ya Tutuba imeeleza kuwa BoT inautahadharisha umma kutojihu sisha na majukwaa na programu tumizi hizo.
“Aidha, Benki Kuu inashirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzifungia programu hizi ili kuepusha umma kutumia huduma za fedha zisizokuwa na vibali vya mamlaka husika,” alieleza Gavana wa Benki Kuu.
Tutuba alieleza kuwa programu hizo hazijakidhi matakwa ya Mwon gozo kwa Watoa Huduma Ndogo za Fedha wa Daraja la Pili wanaotoa huduma za mikopo kwa njia ya kidijiti wa mwaka 2024 uliotolewa na Benki Kuu Agosti 27, mwaka huu.
“Mwongozo huo unalenga kui marisha usimamizi wa Watoa Huduma Ndogo za Fedha Daraja la Pili nchini na kuhakikisha uzingatiwaji wa Kanuni za Kumlinda Mlaji wa Huduma za Fedha, ikijumuisha uwazi, uwekaji wa tozo na riba, njia za ukusanyaji wa madeni na utunzaji wa taarifa binafsi za wateja na kulinda faragha zao,” alieleza.
Soma pia:BOT kuwakwamua waathirika mikopo umiza, kausha damu
Tutuba amezitaja programu tumizi zilizofungiwa ni BoBa Cash, Bolla Kash-Bolla Kash Financial Credit, BongoPesa-Personal Online Loan, Cash Mkopo, Cash Pesa, Cash poa, Cash mama, CashX, Credit Land, Eaglecash Tz, Fast Mkopo, Flower Loan na Fun Loan.
Nyingine ni Fundflex, Get cash, Get loan, Getpesa Tanzania, Hakika loan, Hewa Mkopo, Hi cash, HiPesa, Jokate Foundation Imarisha Maisha, Kopako pa, Kwanza loan, L-pesa Microfinance, Land cash, Loanplus, M-Safi, Mkopo Express, Mkopo Extra, Mkopo haraka na Mkopohuru.
Tutuba alitaja programu nyingine zilizofungiwa ni Mkoponafuu, Mko powako, Money Tap, Mpaso chap loan Mkopo kisasa, Mum loan, My credit, Nikopeshe App, Nufaika Loans, Okoa Maisha Mkopofast, Pesa M, pesa Rahisi, PesaPlus, PesaX, Pocket loan, Pop Pesa, Premier loan, Safe pesa na SasaMkopo.
Nyingine ni Silk loan, Silkda Credit, Soko loan, Sunloan, Sunny Loan, Swift Fund, TALA, TikCash, Twiga Loan, TZcash, Umoja, Usalama Na Uwakika, Mkopo Dk15, Ustawi loan, Viva Mkopo Limited, VunaPesa, Yes Pesa na Zima Cash.
Katika hatua nyingine, BoT imeeleza imeshiriki katika Soko la Jumla la Fedha za Kigeni (IFEM) kwa mujibu wa sera yake ya ushiriki katika soko la Fedha za Kigeni ya mwaka 2023.
Taarifa ya Kurugenzi ya Masoko ya Fedha BoT ilieleza kuwa katika ushiriki huo BoT imenunua Dola za Marekani milioni 23 kupitia mnada wa ushindani kwa kiwango cha wastani cha kubadili sha fedha za kigeni cha Sh 2,655.13 kwa Dola moja ya Marekani. “Lengo la mnada huu lilikuwa ni ku ongeza akiba ya fedha za kigeni kufuatia ongezeko la hivi karibuni la ukwasi wa fedha za kigeni,” ilieleza taarifa hiy