Botswana mthibitishaji madini ya almasi

ULAYA: KUJUMLISHWA kwa Botswana kama mthibitishaji kunaonekana kukusudiwa kuokoa mpango wa utekelezaji wa kusitisha kuagiza almasi Urusi baada ya mataifa ya Afrika kulalamika kuwa uchumi wao utaathirika.

Botswana ni miongoni mwa nchi zinazozalisha almasi barani Afrika, itaungana na Antwerp kama mthibitishaji wa chimbuko la almasi ghafi kwa ajili ya kusafirishwa katika mataIfa ya G7, yaliyopinga uagizaji wa madini ya Urusi kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu.

Ushirikishwaji wa Botswana unalenga kushughulikia wasiwasi wa wazalishaji wa Afrika kuhusu usawa wa kiuchumi. SOMA: Majaliwa ataka sekta ya madini kuwa na tija kiuchumi

Advertisement

Mfumo wa awali wa uthibitishaji ungeshuhudia almasi zote zikipitia kitovu cha almasi cha Ulaya mjini Antwerp kwa ajili ya uhakiki, kwa kutumia teknolojia mpya ya ufuatiliaji.

Lakini wazalishaji wa almasi wa Afrika ikiwemo Angola, Botswana na Namibia, pamoja na kampuni ya uchimbaji ya De Beers, walisema mfumo huo haukuwa wa haki na kwamba ungeathiri uchumi wao.

Mfumo wa ufatiliaji ulipaswa kuanza kufanya kazi kuanzia Septemba Mosi mwaka huu, lakini Umoja wa Ulaya ulichelewesha utekelezaji wake hadi Machi 2025.