Majaliwa ataka sekta ya madini kuwa na tija kiuchumi

DAR ES SALAAM:Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali itaendelea kuiunga mkono sekta ya madini lengo likiwa ni kuona sekta hiyo inakuwa kwa kasi na tija kwa uchumi wa nchi.

Majaliwa ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa Sita wa Kimataifa wa Madini ulioanza leo na unatarajiwa kumalizika Alhamisi.

Majaliwa amesema serikali imeimarisha sekta hiyo kwa kuongeza uwezo wa nishati ya umeme, kuimarisha njia ya usafirishaji kwa kuboresha barabara ya usafirishaji wa madini hayo , kuongeza ndege ili kuimarisha sekta hiyo kwani ni nguzo muhimu kwa ukuaji wa uchumi kwenye nchi yetu.

Advertisement

Majaliwa amesema mkutano huo utaonesha teknolojia rafiki kwa mazingira kwenye uchimbaji madini malengo kuvutia uwekezaji kutoka nje kuja nchini ili iweze kuongeza sekta ya madini kukua hapa nchini, kubadlishana mawazo , kukuza usimamizi bora wa rasilimali tulizonazo za madini kwa manufaa ya taifa letu , kuongeza fursa za ajira na kuboresha ustawi wa jamii unaozunguka kwenye uchimbaji wa madini , kuimarisha ushirikiano kati ya serikali mbalimbali sekta binafsi na wadau wengine.

” Hata hivyo bado nchi yetu hainufaiki na uvunaji wa madini Taifa linakosa manufaa kwa sababu shughuli za uongezaji thamani zinafanyika nje ya nchi ni thahiri kwamba serikali inakosa mnyororo wa thamani wa mapato ambao yangepatikana iwepa yangeongezewa thamani hapahapa nchini kwa kutambua manufaa makubwa ya kiuchumi na kijamii yanayotokana na shughuli za uongezaji thamani inafanyika nchini serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi ikiwemo kufanya mapitio ya sera, sheria na kanuni lakini miongozo mbalimbali ambayo yanabainisha changmoto zilizopo ili kuweza kushughulikia hasa kwenye uongezaji wa thamani wa madini ” amesema Majaliwa.

Majaliwa Amesema serikali itaendelea kutenga bajeti ya kutosha kwa kuongeza mashine za kutosha za uchorongaji wa madini hapa nchini hivyo wachimbaji wajenge imani na serikali katika kuwekeza ili wapate manufaa.

Awali akiongea Waziri wa Madini Antony Mavunde amesema bajeti ya Wizara ya Madini imeongezeka kutoka bilioni 89 mpaka bilioni 231 na fedha hizo zimelekezwa kwenye Taasisi yao ya Geologia na utafiti wa madini (GST) ambapo watajenga maabara kubwa ya kisasa mkoani Dodoma lakini watajenga maabara nyingine mkoa wa kimadini Geita , maabara nyingine mkoa wa kimadini Chunya hivyo itakuwa ukombozi kwa wachimbaji wadogo wa madini na wakubwa ambao wamekuwa wakitumia maabara za ndani na nje ya nchi.

“Rais Samia Suluhu Hassan anakuja kutibu changamoto ilidumu kwa miaka mingi kwa kujenga maabara kubwa na ya kisasa na hivi sasa tumeendelea kuwajenge uwezo watumishi wetu wa maabara kutoka GST tunaye mtaalamu kutoka Finland anaendelea kuwanoa ili tuendelee kutoa huduma yenye uhakika wa hali ya juu ” amesema Mavunde.

Aidha Mavunde amesema serikali imenunua mashine tano za kuchoronga madini amabazo zimegawanywa kikanda huku mashine nyingine 10 zitaingia mwezi wa 11 ambapo zitasaidia wachimbaji wa madni na zitagawanywa kikanda.

Victor Tesha Makamu wa Rais wa Shirikisho la vyama vya wachimbaji wadogo wa madini Tanzania Femata ameiomba serikali kuongeza mashine za uchimbaji madini kwani kwa sasa hivi zipo mashine kumi hivyo kila wilaya zipate mashine moja ,kupata leseni maalumu za wachimbaji wadogo wadogo nchini hivyo wanaweza kuchangua asilimia 40 kwenye pato la nchi pamoja na vyama vya Femata vipate ruzuku kwa wanachama wao .

Mkutano huo wenye kauli mbiu ya “Uongezaji wa thamani kwa maendeleo endelevu wa nchi yetu”