Brandy Rayana kuzindua kitabu cha maisha yake

MSANII wa muziki na filamu kutoka Marekani, Brandy Rayana ametangaza kuzindua kitabu chake cha kumbukumbu za maisha yake ambacho kinatarajia kuzinduliwa rasmi Oktoba 7, 2025.

Kwa mujibu wa tangazo lake, Brandy ameelezea kuwa kitabu hicho kitakuwa na safari ya maisha yake kwa uhalisia wake bila kuchujwa na bila maoni ya vyombo vya habari au wakosoaji.

Brandy anaweka wazi kuwa safari yake haijawa rahisi, kwani changamoto nyingi zimemfinya kuwa mwanamke wa kipekee alivyo hadi leo.

“Kitabu hiki ni zaidi ya hadithi yangu, ni funzo la uvumilivu, matumaini, na kujipata upya nje ya muziki na umaarufu,” alisema Brandy .

Kitabu hiki kinatarajiwa kuwahamasisha wasomaji kuzikabili changamoto za maisha kwa ujasiri na matumaini mapya.

Brandy, alianza kuimba kanisani huko McComb, Mississippi, na kufanikiwa kuwa staa wa kimataifa, anajulikana kwa nyimbo zake kama ‘The Boy Is Mine’, ‘Piano Man’ na ‘Long Distance’, kipindi cha televisheni cha Moesha, na kuwa Cinderella wa kwanza Mweusi.

Mashabiki na wapenda vitabu wanashauriwa kusubiri, ili kugundua hadithi ya kweli ya maisha ya staa Brandy na masomo anayoshea kutoka kwenye safari ya maisha yake na kujigunza.

Habari Zifananazo

Back to top button