Bukoba waitwa kujiandikisha uchaguzi mitaa

KAGERA: MKUU wa Wilaya Bukoba, Erasto Sima amewahimiza wakazi wa wilaya hiyo kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kujiandisha kwenye daftari la mpiga kura ili kutimiza haki yao ya kupiga kura.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kujiandisha kwenye daftari la mpiga kura Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera leo Octoba 11, 2024 DC Sima amesema kuna umuhimu wa kila mwananchi kushiriki zoezi hilo ili apatikane kiongozi wa kumuongoza.

Advertisement

Erick Bozompora ambaye ni ofisa uchaguzi Manispaa Bukoba amesema zoezi la uandikishaji kwenye daftari la mpiga kura katika kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa ndani ya Manispaa ya Bukoba litafanyika ndani ya siku 10 kwenye kata zote 14.

mweyekiti wa Chama cha mapinduzi Mkoa wa Kagera Naziri Karamagi ameshukuru kwa zoezi kuendelea vizuri.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by HABARILEO (@habarileo_tz)