Bunduki za kivita zanaswa kwenye msako
KIGOMA: POLISI mkoani Kigoma imefanikiwa kukamata jumla ya bunduki 16 aina mbalimbali zikihusishwa kutumika kwenye matukio ya uhalifu mkoani humo huku watu 13 wakikamatwa kwa tuhuma za kumiliki bunduki hizo.
Kamanda wa polisi Mkoa Kigoma, Filemon Makungu akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari mjin amesema kuwa bunduki hizo zilikamatwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita ambapo pamoja na bunduki hizo pia risasi 170 zilikamatwa.
Kamanda Makungu amesema katika bunduki hizo zipo Shortgun mbili, AK 47 tatu, Pistol CZ83 Browing moja na gobore 10 ambapo hatua mbalimbali za kuwafikisha mahakamani watuhumiwa hao zimechukuliwa.
Sambamba na hilo Kamanda Makungu amesema katika kipindi cha Januari hadi Desemba mwaka jana jumla ya wahamiaji haramu 941 wamekamatwa mkoani Kigoma wakituhumiwa kuishi na kufanya kazi nchini bila kuwa na vibali.
Wahamiaji hao ambao sehemu kubwa ni raia wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo (DRC) na Burundi kati yao sita walikamatwa wakiwa na nyavu haramu 80 na tayari hatua mbalimbali za kisheria dhidi ya wahamiaji zimechukuliwa kwa polisi kushirikiana na Idara ya uhamiaji mkoani Kigoma.
Aidha, akizungumzia kuhusu dawa ya kulevya Kamanda Makungu alisema kuwa katika kipindi hicho jumla ya tani 1.
6 za madawa ya kulevya aina ya bangi yamekamatwa huku watuhumiwa 56 wakitiwa mbaroni.