Wanne mbaroni mauaji ya mawanafunzi wa IFM

DAR ES SALAAM; Jeshi la Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za mauaji ya James Rogers Temba mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo cha IFM Dar es Salaam ambaye mwili wake ulikutwa unaelea kwenye maji yaliyokuwa yanatiririka katika mto Msimbazi, Dar es Salaam, Aprili 30, 2026.
Taarifa ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Dar es Salaam, Jumanne Muliro imewataja watuhumiwa hao kuwa ni Steven Rogers Chaka, ambaye ni Ofisa Maabara , mkazi wa Bomang’ombe Hai Kilimanjaro, Anna Lema, mfanyabiashara Mkazi wa Tabata Chang’ombe , Twalibu Khamis, mkazi wa Kigogo Kati na Michael John, mkazi wa Kigogo Kati.
“Vipo pia baadhi ya vielelezo ambavyo vinachunguzwa kuhusiana na tukio hilo.Wito wa Jeshi la Polisi kwa wananhi ni kuwa watulivu ili kila aliyehusika kulingana na ushahidi aweze kuchukuliwa hatua za kisheria,” imesema taarifa hiyo.




The analysis presented here offers a valuable framework for understanding the complexities involved. It makes a strong case for re-evaluating our current approaches. Definitely a piece worth revisiting.