Bunge kubana mawaziri

BUNGE limeahidi kupongeza mawaziri wanaofanya vizuri na kubana wasiotekeleza majukumu yao vizuri. Spika wa Bunge, Mussa Zungu ametoa kauli hiyo bungeni Dodoma jana wakati akimpongeza Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Doroth Gwajima kwa utekelezaji mzuri wa kazi zake. “Tutawapongeza mawaziri na watendaji wote wnaofanya vizuri na kuwabana wasiofanya vizuri majukumu yao,” alisema.

Zungu alimpongeza waziri huyo baada ya kusikiliza mchango wa Mbunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa Dar es Salaam Janeth Mahawanga (CCM). Amesema kwa utiifu na uzalendo waziri huyo alimfuata mbunge ili kupata maelezo ya kina kuhusu hoja ili kumsaidia namna ya kuwasaidia wanawake na vijana nchini waliojiunga katika vikundi wanaosubiri kusaidiwa.

“Ninasema haya sababu nilivutiwa na kitendo cha Dk Gwajima kwenda kumuuliza mbunge. Nakupongeza waziri unavyotekeleza majukumu yako kwa utiifu, usahihi na kuhakikisha, azma ya rais ya kutekeleza sera na mipango inafanikiwa na wananchi wanapata majibu sahihi,” alisema. SOMA: Waziri Gwajima atoa wito usalama wa mtoto mtandaoni

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button