Bunge lapitisha bajeti ya Wizara ya Ulinzi

BUNGE limepitisha makadirio na mapato ya mapato na matumizi ya Sh trilioni 2.

98 ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mwaka wa fedha 2023/24.

Wabunge wamefikia uamuzi huo leo Bungeni, Dodoma leo mchana baada ya kujadili mpango wa Wizara hiyo uliowasilishwa na Waziri Innocent Bashungwa mapema leo.

Kati ya kiasi hicho, Waziri ameainisha kuwa takribani Shilingi trilioni 2.8 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida huku kiasi cha Shilingi bilioni 222.8 ni kwa ajili ya kugharamia shughuli za maendeleo.

Ameeleza mambo tisa ambayo Wizara imepanga kuyatekeleza kwa mwaka wa fedha ujao kuwa ni:-

a. Kuliimarisha Jeshi kwa zana na vifaa vya kisasa, mawasiliano na rasilimali watu;
b. Kuimarisha miundombinu mbalimbali katika Kambi za Jeshi na mipakani;
c. Kuendelea kuweka mazingira mazuri ya utendaji kazi kwa Wanajeshi ikiwemo
mafunzo, maslahi, huduma bora za afya na makazi;
d. Kuendelea kulijengea uwezo Jeshi la Kujenga Taifa kutoa mafunzo ya uzalendo,
ukakamavu, umoja wa kitaifa na stadi za kazi kwa vijana wa Mujibu wa Sheria na
wa Kujitolea;
e. Kuendelea kuimarisha Jeshi la Akiba;
f. Kuendeleza na kusimamia rasilimali za Jeshi ikiwemo miradi ya ujenzi hususan
Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa;
g. Kuimarisha mashirika na taasisi za utafiti wa masuala ya kijeshi, ikiwemo
uanzishaji wa viwanda katika sekta ya ulinzi (Defence industries) ili kuzalisha
bidhaa kwa matumizi ya Kijeshi na Kiraia;
h. Kuimarisha ushirikiano na Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya
za Kikanda na nchi nyingine katika nyanja za kijeshi na kiulinzi; na
i. Kuendelea kushirikiana na Mamlaka za Kiraia katika kukabiliana na majanga na
dharura inapohitajika.

Habari Zifananazo

Back to top button