Bunge lapitisha Muswada Sheria ya Ununuzi wa Umma

BUNGE limepitisha Muswada wa Sheria ya Ununuzi wa Umma wa mwaka 2023.

Muswada huo uliwasilishwa mapema leo asubuhi na Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba, ambapo wakati akiwasilisha amesema lengo ni kuweka masharti bora ya usimamizi wa ununuzi wa umma, ugavi na uondoshaji wa mali kwa njia ya zabuni.

“Kwa ujumla, sheria inayopendekezwa inakusudia kutatua changamoto zilizobainika katika utekelezaji wa masharti na taratibu za ununuzi, ugavi na uondoshaji wa mali kwa njia ya zabuni,” amesema Waziri Nchemba.

Advertisement

 

8 comments

Comments are closed.