Burundi yakanusha kuondoa wanajeshi DRC

BURUNDI: SERIKALI ya Burundi imekanusha taarifa za kuwaondoa wanajeshi wake kutoka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo wamekuwa wakisaidia jeshi la Congo kukabiliana na waasi wa M23.

Taarifa hiyo ilitolewa baada ya vyanzo kadhaa kudai kuwa mamia ya wanajeshi wa Burundi walionekana kuondoka eneo hilo na kurejea nyumbani, hasa baada ya waasi wa M23 kusonga mbele, hatua ambayo ingeweza kuwa pigo kwa jeshi la Congo.

Hata hivyo, Msemaji wa Jeshi la Burundi alitupilia mbali taarifa hizo, akisema ni uzushi mtupu na kwamba wanajeshi wa Burundi wanaendelea na operesheni hiyo kwa uwajibikaji mkubwa.

SOMA: Congo yaipelekea Rwanda mahakamani

Juhudi za kusitisha mapigano zinaendelea, huku Rais wa Congo, Felix Tshisekedi, akikutana na Rais wa Angola, Joao Lourenco, mjini Luanda kujadili hali ya usalama inayozidi kuzorota katika eneo la mashariki mwa DR Congo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button