Congo yaipelekea Rwanda mahakamani

DR CONGO: JAMHURI ya kidemokrasia ya Congo (DRC), imewasilisha kesi dhidi ya Rwanda katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu kwa madai ya ukiukwaji wa haki, tuhuma za Congo dhidi ya Rwanda zinahusiana na mzozo ulioikumba eneo la mashariki mwa nchi hiyo tangu 2021, ambako vikosi vyake vimekuwa vikabiliana na waasi wa M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda.

Kesi hiyo iliyowasilishwa mahakamani mwaka 2023 itaanza kusikilizwa rasmi leo Jumatano na Alhamisi ambapo hoja za pande hizo mbili kuhusu mamlaka ya mahakama hiyo na uwezo wake wa kusikiliza ombi iliyowasilishwa na DRC itasikilizwa.

Hayo yamejiri siku chache baada ya marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Mataifa ya Kusini mwa Afrika SADC, kukutana jijini Dar es Salaam Tanzania, kutafuta ufumbuzi wa mzozo huo.

Advertisement

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Mahakama hiyo yenye makao yake jijini Arusha Tanzania, imesema Congo inadai kuwa mzozo huo umesababisha mauaji, uvamizi wa maeneo yake, na watu 520,000 kulazimika kuyahama makazi yao, kuzuka kwa ugonjwa wa kipindupindu na uharibifu wa shule na hivyo kusababisha watoto 20,000 kukosa elimu.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *