MBUNGE wa Jimbo la Bukoba Mjini, Wakili Stephen Byabato amepiga kura kuwachagua viongozi wa Serikali za Mitaa katika kituo cha Chuo Huria Mtaa wa Migera – Nshambya Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera leo.
Byabato amesema kuwa ni haki ya kila mwananchi kumchagua kiongozi anayemtaka huku akiwa mstari wa mbele kuwakumbusha wananchi ambao hawajapiga kura kufanya kufanya hivyo.
“Kupiga kura ni miaka mitano ikipita fursa hiyo huwezi kuipata, nitafanya zoezi la hamasa ya nyumba kwa nyumba kuhakikisha hakuna anayebaki, nawashukuru wananchi kwa mwitikio mkubwa,” amesema Byabato.