CAG: TIC haina programu kukuza uwekezaji

DODOMA — Ripoti Kuu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2023/2024 imesema Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimeshindwa kuandaa na kuwasilisha programu ya kukuza uwekezaji, licha ya kuwa kanuni za uwekezaji za mwaka 2023 zinakitaka kiandae programu hii na kuwasilisha kwa Bodi ya Wakurugenzi kwa ajili ya kuidhinishwa.

Ukosefu wa programu hii unaweza kusababisha kukosa fursa za kimkakati na kukatisha tamaa wawekezaji. TIC inapendekezwa kuhakikisha programu hiyo inatayarishwa na kuidhinishwa na Bodi kwa ajili ya utekelezaji.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button